nmb

nmb

Wednesday, September 19, 2012

Waongoza Wanyama Kazi wanahitaji elimu ya Usalama barabarani

 

 

Wanyama kazi kijijini kama Punda hutumika sana katika kusafirisha Migo kutoka mashambani hadi sokopni au majumbani, wanyama hawa ambao wakati mwingine hukokota matela ya mizigo hutumia barabara hivyo kulazimika kufuata sheria za Usalama barabarani ili kulinda usalama wa wanyama hao na waongozaji wake. Elimu ni muhimu kutolewa kwa watu mbalimbali wanao waongoza wanyama hawa ili kuepusha kutokea ajali wawapo barabarani. Taifa lipo katika maadhimisho ya wiki ya Nenda kwa Usalama ambayo inaadhimishwa Mkoani Iringa huku ikiwa na kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “PAMBANA NA AJALI ZA BARABARANI KWA VITENDO, ZINGATIA SHERIA”.

 

  Vijana na watoto wa Kitongoji cha Kinyenye, Kijiji cha Kipera wilaya ya Mvomero mkaoni Morogoro wakishusha Matofali ya kuchoma yaliyosafirishwa na Punda. Wanyama hawa wamekuwa msaada mkubwa wa usafiri vijijini.

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

AddThis