nmb

nmb

Tuesday, October 9, 2012

Bodi ya utalii TTB yamtambulisha mpishi mkuu kutoka India

Mpishi maarufu Duniani kutoka nchini India Sanjeev  Kapoor (kulia) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam jinsi vyakula vya asili vinavyoweza kuwavutia watalii kwenda kutembelea nchi mbalimbali na hivyo kukuza utalii wa nchi husika huku Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Nchini Dkt. Aloyce Nzuki akimsikilia kwa makini. Mpishi Kapoor amekuja nchini kwa ajili ya kuandaa vipindi vya runinga ambavyo vitahusu mapishi ya vyakula vya  asili ili kutangaza utalii wa kiutamaduni nchini India. 

Mpishi maarufu Duniani kutoka nchini India Sanjeev  Kapoor (kulia) akimkabidhi Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Nchini Dkt. Aloyce Nzuki leo jijini Dar es Salaam kitabu kinachoonyesha aina mbalimbali za mapishi alizoziandaa katika kipindi cha mapishi kijulikanacho kama Khana Khazana kinachorushwa na Televisheni ya Taifa ya India.  Mpishi Kapoor atakuwepo nchini kwa muda wa wiki mbili kwa ajili ya kuandaa vipindi vya runinga ambavyo vitahusu mapishi ya vyakula vya  asili ili kutangaza utalii wa kiutamaduni nchini India.  

Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Nchini Dkt. Aloyce Nzuki akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam kitabu alichopewa na mpishi maarufu Duniani kutoka nchini India Sanjeev  Kapoor  kinachoonyesha aina mbalimbali za mapishi alizoziandaa katika kipindi cha mapishi kijulikanacho kama Khana Khazana kinachorushwa na Televisheni ya Taifa ya India. Mpishi Kapoor atakuwepo nchini kwa muda wa wiki mbili kwa ajili ya kuandaa vipindi vya runinga ambavyo vitahusu mapishi ya vyakula vya  asili ili kutangaza utalii wa kiutamaduni nchini India. 

Baadhi wa wageni waalikwa na mwaandishi wa habari  wakimsiliza Mpishi maarufu Duniani kutoka nchini India Sanjeev  Kapoor (hayupo pichani) akielezea umuhimu wa vyakula vya asili katika sekta ya utalii wa nchi Mpishi Kapoor atakuwepo nchini kwa muda wa wiki mbili kwa ajili ya kuandaa vipindi vya runinga ambavyo vitahusu mapishi ya vyakula vya  asili ili kutangaza utalii wa kiutamaduni nchini India.

Mpishi maarufu Duniani kutoka nchini India Sanjeev  Kapoor (kulia) akisaini  kitabu chake kinachoonyesha aina mbalimbali za mapishi alizoziandaa katika kipindi cha mapishi kijulikanacho kama Khana Khazana kinachorushwa na Televisheni ya Taifa ya India huku Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Nchini Dkt. Aloyce Nzuki akimuangalia.  Mpishi Kapoor atakuwepo nchini kwa muda wa wiki mbili kwa ajili ya kuandaa vipindi vya runinga ambavyo vitahusu mapishi ya vyakula vya  asili ili kutangaza utalii wa kiutamaduni nchini India.

Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Nchini Dkt. Aloyce Nzuki (wa pili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na mpishi maarufu Duniani kutoka nchini India Sanjeev  Kapoor (wa pili kulia) mara baada ya kumalizika kwa mkutano baina yao na waandishi wa habari uliohusu umuhimu wa vyakula vya asili katika sekta ya utalii uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Meneja Mkuu wa Hoteli ya Serena Daniel Sambai na kushoto ni Mkurungezi wa Performance Ltd. Tanzania Runjiv Kapur.
  Picha na Anna Nkinda – Maelezo

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

AddThis