Na Merina Robert, Morogoro
WAKAZI wa Manispaa ya Morogoro wametakiwa kutumia
vizuri kiasi cha maji kinachopatikana kwa sasa, ili kukidhi mahitaji. Tatizo la
upungufu wa maji limesababisha baadhi ya maeneo, wananchi kukosa huduma ya maji
kwa kipindi cha takribani wiki tatu sasa.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jana Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi
na Maji Taka mkoani hapa (MOROWASA), John Mtaita alisema upungufu wa maji kwa
kipindi hiki cha kiangazi ni mkubwa.
“Kuna kuwapo na ukosefu wa maji katika maeneo mengi ya manispaakutokana na
ukame na uharibifu unaofanywa na binadamu katikavyanzo mbalimbali vya maji,
hali inayosababisha ukosefu wa maji,”alisema.
Alisema kiwango cha maji kilichopo hivi sasa ni kidogo kiasi ambachohakiwezi
kukidhi mahitaji ya wananchi waliopo ndani ya manispaa hiyo.
Alisema hali hiyo bado inaendelea kwa sasa kutokana na jua kuendelea kuwaka na
kufanya maji kuendelea kukauka na kusababisha maji kuwa kidogo na hivyo
kuwafanya wananchi kutumia muda mwingi wa kutafuta maji bila mafanikio.
Alisema watu wanaoishi karibu na vyanzo vya maji wamekuwa sehemu ya tatizo
kutokana na kuharibu mazingira na hivyo, kusababisha ukosefu wa maji.
Kwa upande wake mkazi wa Nane Nane, Juma Msisi alisema, maji yamekosekana kwa
muda mrefu sasa katika eneo hilo.
“Nasikitika katika eneo ninaloishi hatuna maji kwa muda mrefu, hii inatufanya
tushindwe kufanya kazi za uzalishaji, tunabaki kutafuta maji umbali mrefu,”
alisema.
Msisi alisema, ipo haja kwa mamlaka hiyo kutafuta miundombinu yakutatua kero
ya maji ambayo ipo kwa muda na kila mwaka bila kupatiwa ufumbuzi.
Chanzo: Mtanzania
No comments:
Post a Comment