nmb

nmb

Saturday, February 23, 2013

Eneo la kumbukumbu ya hayati Sokoine Wami Dakawa pale alipopatia ajali

  Mlinzi wa eneo hilo Bw Mpanda Chalo akimuonyesha mwandishi wa Mtandao huu kumbukumbu ya mnara wa sokoine uliojengwa eneo hilo la Wami dakawa kando kando ya barabara kuu ya Morogoro-Dodoma juzi.
              Mtandao huu umefanikiwa kupata picha halisi ya Sokoine enzi la uhai wake
 lnawezekana umeshaona picha za eneo hili  la kumbukumbu  ya Sokoine,Mtandao huu umechimba chimba na kugundua sehemu ya mnara huo iliyoandikwa nyazifa mbali mbali alizowahi kushika Sokoine kabla ya kifo chake ambazo  zilizochorwa hivi karibuni nyuma ya Mnara huo. na Mtandao huu unakuwa wa kwanza kuzirusha hewani.

    Kwenye gari hili ndipo alipopata ajari waziri mkuu Edward Sokoine mwaka 1984.
                                    NA DUSTAN SHEKIDELE,MOROGORO
WAZIRI Mkuu kipenzi cha watanzani wetu Edward Moringe Sokoine ambaye mwaka 1984 wakati akitoka Bungeni Dodoma  na kurejea jijini Dar es salaam alipofika eneo la Wami Dawaka wilaya ya Mvomero Mkoani hapa gari lake liligonga uso kwa uso na gari lingine lililokuwa likitokea Morogoro mjini ambapo kwenye ajari hiyo  Sokoine pekee ndiye aliyepoteza maisha.

 Kufutia hali hiyo serikali iliamu kujenga mnara kwenye eneo hili kwa lengo la kumkumbuka warizi mkuu huyo kiboko cha wahujumu wa Uchumi.

Juzi mwandishi wa Mtandao huu aliamu kutembelea eneo hilo na kwamba mlizi wa eneo hilo Bw Mpanda Chalo alipohojiwa alidai kwamba kwa sasa serikali imeamu pia kujenga shule ya sekondari nyuma ya mnara huo kwa lengo  la kumuezi kiongozi huyo muadilifu.

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

AddThis