nmb

nmb

Friday, April 5, 2013

Maandalizi ya Ngorongoro Half Marathon, “Mbio za mapambano dhidi ya Malaria” yakamilika Kufanyika karatu kesho Aprili 6. kupambwa na Barnaba


  
Mwakilishi wa kampuni ya Tigo, Bw Joseph James akikabizi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi millioni kumi na sita (Tsh, 16,000,000) kwa wandaaji wa mashindano hayo taasisi ya Zara Charity  (Leila Ansell)

Tigo Tanzania kwa kushirikiana na taasisi isiyo ya Kiserikali ya  ZARA Charity, taasisi tanzu ya kujitolea ya kampuni ya Utalii ya ZARA Tanzania Adventures ambayo husaidia  shughuli mbalimbali za kijamii kwa kujitolea ndio waandaji Mbio hizo za za Sita za Nusu marathon (kilomita 21.1) zijulikanazo kama ‘Tigo Ngorongoro nusu Marathon’ zitakazofanyika  kesho jumamosi ya Aprili 6, mwaka 2013.

Mashindano hayo ya mbio kwa mwaka huu yamebeba ujumbe wa ‘Mbio za Mapambano dhidi ya Malaria’ yatafanyika katika mji mdogo wa Karatu mkoani Arusha

 
Mnamo mwaka 2010, kampuni ya  Zara Tanzania adventures ilianzisha na kuwa mdhamini mkuu wa  mbio za watoto za kilomita tano zilipewa jina la ‘Ngorongoro Run: Kids’ Fun Run’, mbio ambazo zimetia chachu zaidi mbio hizo za Ngorongoro Marathon.
Zaidi ya wakazi  5,000 wa Karatu wanashiriki na kuzifurahia sana mbio hizo ambapo pia hupata fursa ya kujifunza masuala mbalimbali ya mapambano dhidi ya malaria.

 Mbio za Ngorongoro Marathon mwaka huu ni za kipekee sana kwani zinajumuisha ushindanishaji wa makampuni mbalimbali ulioandaliwa na kampuni ya mtandao wa simu za mkononi Tigo  yatakayofanyika kabla ya kuanza kwa mashindano hayo ambapo mshindi ataibuka na kitita cha dola za kimarekani  20,000 ambazo atajitolea kwa taasisi yeyote yenye uhitaji atakayoichagua.

Ufunguzi wa mbio hizo unatarajiwa kuhudhuriwa na zaidi ya watu  3000 ambapo Mgeni Rasmi atakayefungua mbio hizo anatarajiwa kuwa Naibu waziri wa Mali asili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu.

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

AddThis