nmb

nmb

Friday, May 24, 2013

Rais Obama wa Marekani kufanya ziara katika mataifa matatu ya Afrika ikiwemo Tanzania.

president-barack-obama

Rais Barack Obama wa Marekani anatarajiwa kuzuru bara la Afrika mwezi ujao ambako atatembelea mataifa ya Senegal, Afrika kusini na Tanzania.
Kwa mujibu wa taarifa ya msemaji wa Ikulu ya Rais nchini Marekani Jay Carney, rais Obama amepangiwa kufanya ziara hiyo kati ya tarehe 28 mwezi ujao hadi tarehe 3 mwezi Julai ambako atakutana na viongozi wa serikali, biashara na wa mashirika ya kijamii kwa lengo la kuhimiza amani na ustawi wa bara Afrika.

Taarifa hiyo imefafanua kuwa Rais huyo wa Marekani atasisitiza umuhimu wa uhusiano kati ya Marekani na nchi za Afrika ikiwemo kupanua ukuaji wa kiuchumi, uwekezaji na biashara pamoja na kuboresha asasi za kidemokrasia.
Mara ya mwisho kwa rais Obama kutembelea nchi ya bara Afrika ni mwaka 2009 alipozuru Ghana.

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

AddThis