nmb

nmb

Thursday, May 9, 2013

Ufahamu Uchomaji Nyama wa Mila ya Jamii ya Kifugaji Wilayani Simanjiro


Pichani ni aina ya uchomaji nyama wa jamii ya Kimasai kama ulivyokutwa na Camera yetu mnadani mjini Orlkasmet Wilayani Simanjiro mkoa wa Manyara. Uchomaji nyama wa aina hii ni mzuri kwa afya ya mlaji kama tulivyopewa maelezo na wenyeji wetu.
Wakazi wa  Arusha mjini ambao walitembelea Wilayani Simanjiro kwa shughuli zao za kijamii wakisubiri nyama iive kwa ajili ya kupata Mlo wa mchana kama walivyokutwa na Camera yetu Orlkasmet Wilayani Simanjiro. Huku bei ya mguu wa Mbuzi ikiuzwa kati ya Shilingi 15,000-13,000.
Wakazi wa Arusha wakijinoma maini ya Mbuzi yaliyochomwa kimila ya jamii ya kifugaji kama walivyokutwa na camera yetu kwenye mnada katika Soko la jamii wafugaji wilayani humo.
Mnyama aina ya Mbwa akisubiria mabaki nyama ambazo zinabakizwa na walaji katika eneo hilo.

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

AddThis