nmb

nmb

Saturday, April 13, 2013

MATANGAZO YA MZUNGUKO WA NYUMBU YANAYORUSHWA NA CCTV YAHAMASISHA UTALII NCHINI

1. 
Mkurugenzi wa Idara ya Utalii , Wizara ya Maliasili na Utalii nchini Bw. Ibrahim Mussa (kushoto) akizungumza na Makamu Mwenyekiti wa Wizara ya Utalii ya China Bw. Zhu Shanzhong juu ya masuala mbalimbali ya uhusiano baina ya nchi hizi mbili hususan katika sekta ya utalii wa Tanzania katika soko la China.
2 
Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi (kushoto) na Kaimu Mhifadhi wa   Mamlaka ya Ngorongoro Bruno Kawasange wakifuatilia mazungumzo hayo.
3 
Balozi wa Tanzania nchini China Philip Marmo (kulia) na Mbunge wa Ngorongoro  Mhe. Kaika Telele wakifuatilia mazungumzo baina ya serikali ya Tanzania na China kuhusiana na sekta ya utalii nchini.
4 
Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Dk. Aloyce Nzuki (kulia) na Mkurugenzi Msaidizi wa Malikale John Kimaro wakifuatilia mazungumzo hayo kwa umakini.
5 
Viongozi wa Serikali ya China wakifuatilia majadiliano. (Picha zote na mdau Pascal Shelutete, TANAPA)
6 
Mkurugenzi wa Idara ya Utalii Ibrahimu Mussa (kushoto) akipokea zawadi maalum ya stempu mbalimbali za China kutoka kwa Makamu Mwenyekiti wa Wizara ya Utalii nchini China  Zhu Shanzhong mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo yao.
7 
Mkurugenzi wa Utalii Ibrahimu Mussa na Balozi Philip Marmo wakiwa na Makamu Mwenyekiti wa Wizara ya Utalii ya China Bw. Zhu Shanzhong
…………………………………………….

Pascal Shelutete, Beijing
Matangazo ya moja kwa moja ya Mzunguko wa Nyumbu wahamao katika Hifadhi ya Serengeti katika Televisheni ya Taifa ya China yameongeza mwamko wa wachina kutembelea Tanzania kama watalii. Haya yalisemwa jana na Makamu Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Utalii ya China Zhu Shanzhong alipokutana na ujumbe kutoka Tanzania jijini Beijing China.
Shanzhong alisema kuwa Hifadhi ya Serengeti ambapo vipindi kadhaa vimesharushwa tangu mwezi januari mwaka huu nchini China, inaendelea kupata umaarufu mkubwa  miongoni mwa wananchi wa China na kuelezea matarajio yake kuwa matangazo haya yataweza kuongeza idadi ya watalii nchini katika muda mfupi ujao.

Alisema kuwa ziaraya hivi karibuni iliyofanywa na Rais wa Ji Xinping nchini imeendelea kuitangaza Tanzania nchini China na kuongeza kuwa upekee wa vivutio vya utalii  ni mtaji mzuri unaopaswa kutumika vizuri kutangaza utalii na hivyo kuongeza pato la taifa.
Mapema Makamu Mwenyekiti huyo alieleza haja ya kuwepo kwa ushirikiano wa karibu baina ya sekta za utalii kwa nchi hizi mbili na kutaka kuandaliwa kwa rasimu ya Hati ya Makubaliano itakayobainisha maeneo muhimu ya kushirikiana kwa kuwa na mipango thabiti ya muda mrefu na mfupi.

Katika mkutano huo, Shanzhong aliomba ridhaa ya Tanzania kuridhia ombi la China la kuanza kutumia kwa lugha ya kichina kuwa mojawapo ya lugha rasmi zitakazotumika katika vikao vya Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii. Alieleza kuwa nchi yake imepeleka ombi hilo makao makuu ya shirika hilo ambayo yanahitaji kuungwa mkono na zaidi ya nusu ya nchi wanachama wa shirika hilo.Ujumbe wa Tanzania unaoongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya Utalii Ibrahim Mussa uliahidi kuwa Tanzania itaunga mkono ombi hilo kabla ya kufanyika kwa mkutano mkuu wa UNTWO mapema mwezi Agosti mwaka huu nchini Zimbabwe na Zambia

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

AddThis