nmb

nmb

Thursday, March 27, 2014

TIGO NGORONGORO MARATHON‏

Meneja Mawasiliano wa Tigo John Wanyancha akizungumza na waandishi wa habari mapema leo wakati wa kutangaza udhamini wa kampuni hiyo katika mbio za 'Tigo Ngorongoro Marathon' zitakazofanyika 19 Aprili 2014 wilayani Karatu, Ngorongoro - Arusha. Kushoto ni Mratibu wa mbio hizo, Datus Joseph, kutoka kampuni ya utalii ya Zara Tours.

Mratibu wa Matukio, Datus Joseph, kutoka kampuni ya utalii ya Zara Tours akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mbio hizo mapema leo.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Tigo Ngorongoro Marathon kuchangisha fedha kwa ajili ya kukumbana na Malaria nchini
Dar es Salaam, 17 Machi  2014 – Mwaka wa saba wa ‘Tigo Ngorongoro Half Marathon’ iliyopewa kauli mbiu ya “Kimbia kuikabili Malaria” itafanyika Jumamosi ya 19 Aprili 2014 wilayani Karatu, jijini Arusha. Mbio hizo za kila mwaka inategemea kuwavutia wanariadha 3000 wa kitaifa na kimataifa, Tigo ilitangaza leo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Meneja Mawasiliano wa Tigo John Wanyancha, alisema kwamba Tigo Ngorongoro Marathon ni fursa ya kuhamasisha jamii kuhusu jinsi ugonjwa wa Malaria unavyoathiri watu milioni 300 mpaka 500 duniani, asilimia 90 wakiwemo barani Afrika.
“Malaria inaua zaidi watu milioni moja kila mwaka. Nchini Tanzania mtu mmoja anafariki kwa ugonjwa wa malaria kila baada ya dakika 10. Mbio za mwaka huu inahusisha pia harambee yakujenga kituo cha hospitali,” alisema Wanyancha.

Mwaka wa 7 wa mbio hizi za Tigo Ngorongoro Half Marathon inaambatana na maadhimisho ya Siku ya Malaria inayoadhimishwa tarehe 25 Aprili kila mwaka. Tukio hilo, kutokana na maelezo ya Wanyancha inategemewa kuzinduliwa na Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu kama mgeni rasmi.
Tigo inashirikiana na moja ya makampuni ya utalii yanayoongoza nchini kwa jina la Zara Tanzania Adventures, katika kuandaa mashindano haya, ambapo fedha  zitakazopatikana zitatumika kununua na kugawa neti za mbu, pamoja na kununua dawa za malaria ambapo zitagawiwa mahospitalini Arusha bure.
Fedha zitakazochangishwa pia mwaka huu zitatumika kukarabati vituo vya afya vilivyopo pamoja na kujenga kituo kipya cha afya kitakachoanzishwa Ngorongoro pamoja na shule ya awali katika vijiji tofauti tofauti kwa gharama ya shilingi milioni 160 jumla, alisema Wanyancha.

“Mbio za Tigo Ngorongoro half marathon sio tu  burudani kwa watu watakaoshuhudia bali ni sehemu nzuri sana yenye kuhamasisha kuhusu namna ya kujikinga na kutibu ugonjwa wa malaria kwa jamii inayozunguka maeneo ya Monduli na Arusha kwa ujumla,” alisema.

Mbio hizi zinawapa fursa wanariadha kukimbia katika sehemu moja yenye vivutio vya kipekee duniani, kutoka kivutio cha Ngorongoro mpaka jiji la Karatu. Mbio za mwaka huu pia inahusisha mashindano ya makampuni ya kilomita 5 kwa makampuni wenye nia yakuchangia katika harambee hiyo.
Kutokana na maelezo ya Mratibu wa Mbio hizo, Datus Joseph, kampuni zinazaodhamini mbio hizi katika ngazi za mashindano ya makampuni ni SBC Tanzania Ltd, CHUCHU, BG Tanzania, Hans Paul, Mberesero Lodge Tented Camps, Afrika-Safari, Orange gas na BIL

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

AddThis