nmb

nmb

Wednesday, September 26, 2012

SIKU YA UTALII DUNIANI MAADHIMISHO KUANZA MKOANI IRINGA

 
Afisa habari za utalii ofisi ya TANAPA kanda ya kusini Risala Kabongo akifafanua jambo kwa   waandishi wa habari Leo
 
Mwenyekiti wa kamati ya Wiki ya Utalii Iringa Adam Swai akifafanua jambo kuhusu maadhimisho ya siku ya utalii duniani
Siku ya Utalii Duniani huadhimishwa tarehe 27 Septemba ya kila mwaka. Lengo lake ni kuhamasisha na kuweka uelewa kati ya jamii za Kimataifa kuhusu umuhimu wa utalii na thamani yake kijamii, kisiasa, kitamaduni, na kiuchumi.

 Afisa habari wa TANAPA kanda ya kusini Risala Kabongo ameeleza kuwa maadhimisho haya yatatoa fursa ya majadiliano kwa wadau wa sekta ya utalii yatakayo lenga katika kukuza uhusiano wa kibiashara kati ya watoa huduma na bidhaa katika sekta ikiwa ni pamoja na Hifadhi ya taifa ya TANAPA, Ruaha, hifadhi ya udzungwa kitulo na sekta binafisi, watu wa madawa na fursa imetolewa kwa vyuo vikuu ili wapate nafasi ya kujitangaza na kuzungumzia masuala ya taaluma wajasiliamali , wazalishaji wa vyakula na mahoteli.

Siku hii ya utalii kitaifa inaadhimishwa mwanza ambapo kilele chake kitakuwa siku ya tarehe 27 Kauli mbiu ya mwaka huu inasema (Tourism and sustainable energy powering sustainable development) utalii endelevu na matumizi endelevu ya nishati kwa maendeleo endelevu

Wananchi wa mkoa wa Iringa na wadau mbalimbali wamehamasishwa kufika katika maonesho hayo yatakayoanza siku ya  tarehe 25 hadi 27 katika uwanja wa Samora

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

AddThis