Hapo ni wenyeji wakipiga makofi na kumzunguka kwa furaha kwa neema iliyoletewa na kakakuona
Na shuhuda mmoja huko kilwa
Usiku mlinzi aliyejawa hofu
alinizinduwa (amsha usingizini) baada ya kuona kiumbe wa ajabu. Alikuwa ngaka (kakakuona)
mwenye uzito wa kilo 32.... Hata wanasayansi wanajua machache kuhusu mnyama
huyo aonekanae kwa nadra sana!
Niliwapigia simu idara ya
wanyama pori waje wamchukue ili wakamhifadhi.Ukatokea mzozo na wazee wa kijiji
kwamba ni lazima afanyiwe ada ya kiasili kwani ugeni wake huyo ni muhimu kuliko
hata wa mgeni yoyote yule bora.Hivyo kakakuona akawekewa mkeka mpya, vikapangwa
vitu muhimu vya kutabiriwa ili aweze kuabiri.
Jembe, panga, kibiriti, maji,
hela, mahindi, ufuta....baada ya mimi kusema tuweke mtungi wa gesi kwani
hapa kwetu gesi asilia ndio zao kuu kwetu na mimi ndio biashara yangu wazee
wakasema hayo ni mambo ya kizungu lakini baadae wakakubaliana na wazo langu la
kuweka mtungi wa gesi. Kama vile Ngaka alitaka kutupa huo ujumbe moja kwa moja ...paaarrrrr
akikimbia hadi kwenye mtungi wa Gesi!! Akaviacha vitu vingine vyote! Wala
havikukumshughulisha...amini usiamini baada ya Ngaka kuzunguka akikitupia macho
kitu kimoja kimoja akaamua kuondoka na kisha kurudi kama aliesahaua kitu....
moja kwa moja mpaka kwenye mtungi wa gesi akatoa ulimi wake na kubusu mara
mbili sisi tukapigwa butwaa na kupiga makofi tukiashiria neema ya gesi kwenye
wilaya yetu. Hongera kilwa na Natural Gas discoveries Ngaka ametabiri hivyo.....
Habari na tabianchi.blog
No comments:
Post a Comment