Warembo
wanaoshiriki shindano la Redds Miss Tanzania 2012, wakiwa katika picha
ya pamoja Oktoba 7, 2012 wakati warembo hao walipo tembelea Hifadhi ya
Mlima Kilimanjaro na kupata maelezo na kuzungumza na watalii na wapanda
mlima huo. Warembo 29 na viongozi wa Kamati ya Miss Tanzania wapo Kanda ya Kaskazini kutembelea vivutio vya utalii na kuhamasisha utalii wa ndani. Mbali
na kutembelea hifadhi hiyo lakini warembo hao walishiriki katika
tamasha la michezo kwaajili ya kuchangia fedha na vitu mbalimbali kwa
watoto Yatima mjini Arusha. Oktoba 8 warembo wanaendelea na ziara yao ikiwa ni pamoja na kutembelea kituo cha Redio cha RADIO 5 cha mjini Arusha.
Washiriki
wa Redds Miss tanzania 2012 wakiwa katiak picha tofauti tofauti wakati
wakiwa katika eneo la Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro KINAPA.
Warembo wakizungumza na mmoja wa Wasaidizi wa watalii wanao panda mlima Kilimanjaro.
baadhi ya warembo wakipiga picha na baadhi ya viongozi wa Kamati ya Miss Tanzania
Warembo wakizungumza na mmoja wa Wasaidizi wa watalii wanao panda mlima Kilimanjaro.
Warembo wakiwa wakiwa katika eneo la maegesho ya magari KINAPA
Wakielekea eneo la kupata taarifa mbalimbali za Mlima Kilimanajaro
Wakipiga picha na baadhi ya watalii waliowakuta hapo.
Warembo
wa Redds Miss Tanzania wakimsikiliza Afisa Mhifadhi wa KINAPA, Eva
Malya aliyekuwa akiwapa taarifa mbalimbali juu ya mlima huo.
Warembo wakiwa na nyuso za furaha wakiendelea kupata maelezo juu ya mlima
Hapa sasa walibeba mabegi ili wapande Mlima.
No comments:
Post a Comment