Kwa hali ya
kawaida utaona ni ngumu kuamini kwamba kitu kama utamaduni kinaweza kuwa chanzo
kikubwa cha uchumi kukua katika nchi husika.
Nchi ya
Rwanda imekuwa moja kati ya nchi baarani Afrika ambayo imefanikiwa kukuza na
kuendeleza utamaduni na sanaaa mbao tayari imekuwa ikichangia kalibia asilimia
60 ya mapato ya nchini na kuwapatia ajira vijana kwa urahisi.
Mapato haya
yamekuwa yakitokana na fedha za kigeni
ambazo wamekuwa wakitoa watalii kutoka nje ambao hasa wamekuwa wakihamasika
kununua vitu vizuri vya asili ambavyo vinatengenezwa kiasilia na wasanii wa
sanaa za utamaduni nchini humo.
Mbali
na kuteka soko la watalii wamekuwa na vivutio vya asili ikiwemo
vyakula na ngoma.Taasisi zinazohusika na mambo ya utalii wamekuwa mstali
wa mbele kutangaza vivutio hivyo ndani na nje ya nchi ukilinganisha na
sisi wabongo ambao tunavivutio lukuki na tumeshindwa kunufaika navyo.
No comments:
Post a Comment