Ni Mjasiriamali aliyewekeza nguvu na uelewa wake wa mambo ya wanyama
pori na mazingira yao kwa kuwaelimisha wageni wanaungana nae. Hujulikana
kama Mwananyika lakini hivi karibuni amepewa jina la Drogba (wanadai ya
kuwa kafanana na Drogba yule mwanasoka maarufu). Anapatikana kwenye
kijiji cha Mloka huko Rufiji, kijiji ambacho kipo nje ya pori la akiba
la Selous.
Shughuli yake kubwa inayompa ugali wake ni kuongoza wageni kwenye safari
za matembezi. Mwenyewe hujigamba kwa kuziita true Africa walking
safari. Daima anapokuwa mzigoni huwa anavaa mavazi ya asili kabisa
ambayo kayatengeneza kwa magome ya miti huku akiwa amebeba ngao, mkuki
na kikapu chake cha kuobebea mitishamba.
Safari zake huwa zinafuata barabara na wakati mwingine huacha barabara
na kuingie mapori. yeye huzunguka na wageni wake nje ya hifadhi japo pia
wanyama wa porini (wakali na wapole) wanakuwepo. Kwa ajili ya tahadhari
na usalama, anapofanya safari za miguu na wageni wake daima huwa
anaambatana na askari toka kwenye campsite waliofikia wageni wake ambaye
huwa na bunduki kwa ajili ya tahadhari. Angalia picha ya pila juu,
upande wako wa kushoto utamuona askari mwenye riffle. Elewa ya kwamba
safari za matembezi ndani ya hifadhi, mgeni husindikizwa na Ranger wa
Maliasili na guide wake au ranger peke yake. Drogba yeye anacheza nje ya
hifadhi.
Safari zake huwa na vituo vingi ndani yake na kwenye kila kituo kuna
jambo ambalo huona ni vyema wageni wake wapate kulifahamu. wakati
mwingine mkiwa nae safarini mnaweza kukutana na wanyama na wakati
mwingine safari zake zikawa ni mafunzo ya wanyama na mazingira yao
zaidi.
Mgeni hufundishwa namna ya kutambua nyayo za wanyama mbalimbali ambazo huwa wanakutana nazo wakiwa safarini.
Safari ikiendelea na vituo vikiwemo ndani yake
Ahsante ya picha Mdau Rajab - Wildness Safaris Tanzania
No comments:
Post a Comment