nmb

nmb

Tuesday, December 25, 2012

KEEP LEFT CHA MSAMVU CHAFANANISHWA NA NIYONZIMA WA YANGA


Mzunguiko huu wa barabara uliopo maeneo ya Msavu umepachikwa jina la Kiungo wa Yanga Mnyarwanda Haruna Niyonzima kutokna na kugawa mikoa mbali mbali ya nchi ya Tanzania.,ambapo unapofika kwenye mzunguko huo utakutana na vibao vinavyokueleka mikoa hiyo



Mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera akihojiwa na Mtadao huu kuhusina na mambo mbali mbali yanayo husu mkoa huo uliopambwa na Milima ya Uluguru.


                   

HAPANA shaka yoyote kwamba ukitoka jijini Dar es salaama na kuelekea mikoa mbali mbali ya nchi ya Tanzania na nchi jirani ni lazima uzunguke mzunguko wa barabra uliopo maeneo ya Msamvu mkoani Morogoro.


Kufuatia uzuri wa mkoa huo  uliosifiwa sana na mwanamuziki nyota barani Afrika  ambaye kwa sasa ni marehemu Mdarak Mwishehe pia wenyeji wa mkoa huo unaoundwa na makabira kadhaa likiwemo kabila kuu la Waluguru,Wapogoro,wasagara, wakagulu,wazigua wa Turiani  na Wakutu,ambao kwa pamoja walizidisha chachu hiyo kwa kusema kwamba "Morogoro ni mji kasoro bahari''



Baadhi ya watu wa makabila hayo wanaofanya kazi stendi kuu ya mabasi ya Mkoani Morogoro iliyopo maeneo ya Msamvu,kutokana na umuhimu ya Keep Left cha Msavu wamekipajika jina la Kiungho nyota na ghari wa timu ya Yanga Mnyarwanda Harun Niyonzima.


Keep Left hicho kimekuwa kiungo muhimu kwa mikoa mbali mbali ya Tanzania.ambapo ukitoka Dar es salaama kuelekea mikoa ya Dodoma,Singida,Tabora,Shinyanga,Mwanza, Mara, Bukoba,Kigoma na nchi jirani kama vile Malawi lazima uzunguke mzunguko huo wa Msavu.

Vile vile ukitaka kwenda Mikoa ya lringa,Mbeya na nchi jirani kama vile Zambia na Afrika kusini ni lazima pia uzunguke mzunguko huo wa Msamvu,kama vile haitishi ukitoka kwenye mikoa hiyo kueleka jiji la Dar e salaam na mikoa ya kasikazi kama vile Arusha,Tanga Moshi na nchi jirani ya Kenya pia ni lazima uzunguke mzunguko huo'

Hivyo Keep Left hicho kimekuwa kiungo muhimu kinachounganisha mikoa mbali mbali ambapo kwa manti hiyo wapega debe hao wa stendi ya Msamvu wameamua kikipachika jina na Niyonzima mabyeni ni kiungo muhia wa timu ya yanga na timu Yanga yenye masikiani yake mitaa ya Twiga na Jangwani jijini Dar Dar salaam

Kwa sasa viongozi wa mkoa huo wakiongozwa na Meya  wako kwenye mikakati kabambe ya kuhakika miaka ya hivi karibuni mkoa huo unapewa hadhi ya jiji.
Habari na DUSTAN SHEKIDELE

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

AddThis