nmb

nmb

Friday, July 20, 2012

Watalii maelekezo mazuri ya kufikia vivutio vya utalii

 
wanafunzi wa shahada ya utalii chuo kikuu cha Dodoma


Na Charles Kayoka

SEKTA ya utalii inaingiza kipato kiwango kikubwa sana. Kwa mfano, Tanzania, sekta hiyo  pengine ndio inayoingiza mapato makunwa kuliko vyanzo vingine vya ndani.


Lakini ukilinganisha na baadhi ya nchi nyingine, utabaini kwamba  sisi bado tuna mengi ya kufanya, mojawapo likiwa ni  kuhakikisha miji yetu inakuwa ya kuvutia kwa ajili ya watalii wa ndani na nje.


Kutokana na hali hiyo napendekeza mambo machache kuhusiana na suala hili. Mambo yanayopaswa kuvutia watalii katika miji yetu ni lazima iwe na vilelezo vya kuwaongoza watalii wapi wanakwenda na wajifunza nini.


Nakumbuka rafiki yangu mmoja ambaye alikuwa mgeni alitaka kwenda Morogoro, lakini kabla ya kwenda huo aliniomba nikienda huko nirudi na ramani ya mji huo. Nilipofika kule nikaenda katika halmashauri, lakini sikupata  aina yoyote ya ramani. Tunapaswa  kuwa na mifumo katika kompyuta ambayo itamsaidia mtalii kupitia simu yake ya mkononi kujua yupo katika eneo gani, na ni wapi anataka kwenda.


Nilipokuwa Arusha, nilishangaa, kwa mfano, kuna matangazo ya vivutio vya utalii vya Gombe, Mikumi na kadhalika, lakini hakuna maelezo ya vivutio vya utalii ndani ya mji, na wapi mtalii anaweza kwenda kupata vitu vya kununua kama kumbukumbu, yaani hata kibao cha barabarani hakuna.


Tunapaswa kutambua kwamba mtalii anakuja Tanzania kujifunza historia, utamaduni, na mambo mengine mbalimbali. Sasa ili mtalii apate cha kuzungumia baada ya kurejea kwao au apate sababu ya kurudi tena  Tanzania, sekta ya utalii inapaswa kuandaa mazingira mazuri ya vivutio na maelekezo yan kufika kwenye vivutio hivyo.


Maofisa wa vivutio mbalimbali wanapaswa kumwelekeza maeneo ya kiutamaduni na kihistoria ambayo atayabeba kwa picha au sauti na kurudi nayo nyumbani.


Katika miji yetu mikuu hakuna vitabu vya picha, haina maduka ambako utapata muziki wa kijadi wa kiafrika hasa, lakini badala yake katika maduka muziki utapa muziki wa bongo fleva ambazo zinafanana na nchi wanakotoka watalii wa kigeni. Ni wapi atapata muziki wa kimakonde, kipogoro au kingindo .


Katika Jiji la  Dar esSalaam, kwa mfano, ni mji wenye historia  ya Wazaramo, Waarabu, Wajerumani, Wahindi na Waingereza, lakini ni wapi mtalii anakwenda kupata japo picha inayoonyesha utajiri wa kihistoria wa Kitanzania.


Hakuna ubishi, katika nchi yetu tumekuwa tukiona jinsi majumba ya kihistoria jinsi yanavyobomolewa wa kasi.


Usafi kwetu ni tatizo kubwa sana. Mtalii angependa kwenda sehemu yote ya mji kwa kuwa anataka kuuona mji kwa upana wake, na kujifunza maisha. Lakini sidhani kama mtalii atapenda kurudi tena akifika sokoni Buguruni, Tandale au Mabibo, achilia mbali Kariakoo ambako ni kitovu cha uchafu, uvundo na kunuka.


Katikati ya jiji, uchafu ni kitu cha kawaida, ni jambo la kawaida kuona chemba za vyoo zimezibuka na majitaka yanatiririka, licha ya sasa wanajitahidi.  Ni jambo la kawaida kuona mji ukiwa na rundo kubwa la uchafu.


Katika ardhi yetu, sekta ya utalii inapaswa kuweka vionjo vya kisanaa, lakini vya kuvutia. Katika majengo na barabara tunaweza kujenga vionjo ambavyo huvutia watu kutembea. Nadhani upangaji wa miji usiishie tu katika kukamilisha nia ya matumizi, ni lazima kufikia viwango vya vionjo.

Awali niliwahi kusema kwamba katika picha ya kaburi kumejengewa vionjo ambavyo watu wangependa kutembelea tena na tena. Niishie hapa kwa leo.

Wasomaji wanaweza kusema kwamba wenzetu wanafanikiwa kwa sababu wana utajiri wa fedha, sio kweli kabisa, kama ni fedha sisi tunazo nyingi kuliko wao.

Ila katika nchi zilizoendelea kiviwanda, wanajua namna ya kuzitumia kwa faida ya umma na wanawajibika. Wanajua kwamba wasipofanya hivyo biashara itakufa. Kuwajibika na kupenda kuacha historia- legacy, ndio sifa ya wenzetu.

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

AddThis