nmb

nmb

Monday, May 6, 2013

EPISODE YA 54 – “TAMTHILIA YA MARA CLARA” – GARY APATA DHAMANA

MaraClara
Amante apata fahamu na kuongea na Alvira, wote waombana msamaha na kurudiana, lakini kwa upande wa Gary hali bado ni tete, kwani anampigia simu Clara ili amdhamini kutoka polisi.
Clara afanikiwa kumtoa baba yake polisi, lakini anajaribu kumshinikiza wahamie nyumba nyingine kwani hiyo ni mbaya, lakini Gary hajakubaliana na wazo hilo kabisaaa!.


Gary anampigia simu Alvira na kumtaka wakutane kwa maongezi lakini, Alvira anakataa na kusema yeye ndio chanzo cha mambo yote yaliyotokea, akaongeza kwa kusema “nenda kuzimu”.
Clara aenda hospitali kuomba wazuie kesi ya baba yake Gary isipelekwe mahakamani, lakini maombi hayo yanatupiliwa mbali na familia ya Amante, aondoka hospitali kwa hasira.

MARA na SUZAN wanaenda kumuona mama yake Gary mwenye ugonjwa wa kupooza, wanamuuliza kama Clara anajua au anashiriki katika maovu ya Gary? Pia bibi huyo anaomba waondoke naye, wanafanikiwa kutoroka nae na kutokomea kusikojulikana.

Gary anarudi na kumuuliza mlezi wa mama yake (Mrs. David) kwa ukali huku akimkaba shingoni, “mama yangu yukowapi?” Anaamua kumfukuza ili akamtafute mama yake hadi ampate kwani asipompata atamuua. Gary na Clara wanaamua kwenda kuripot polisi, lakini polisi wanamwambia hawawezi kumtafuta mtu yeyote anayedhaniwa kupotea hadi masaa 24 yapite. Gary anakasilika na kuanza kujibizana na polisi, lakini Clara anamwepusha na kuondoka kituoni hapo.

MARA na Suzan wafanikiwa kumtorosha mama yake Gary na kwenda nae katika nyumba mpya ya Alvira, huko nyumbani bibi huyo anaanza kupata nafuu ya kuweza kuongea. Amante anatoka hospitali na kujumuika na familia yake upya, lakini Amante anaanza kumuuliza mama yake Gary kuhusu maovu ya mwanae ili apate ushahidi wa kumtupa jela.

Gary, Clara wote wanakutana na familia ya Amante uso kwa uso, sasa nini kitatokea kati yao?
[Mwandishi Vikta Machota]…..itaendelea

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

AddThis