Mkurugenzi
wa Bodi ya Utalii nchini Tanzania TTB Dk Aloyce Nzuki wa tatu kutoka
kushoto akiwa katika picha ya pamoja na watanzania hao wakiwa wameshika
vyeti vyao kushoto ni Wilfred Moshi, Respicius Baitwa wa pili kutoka
kulia na Juma K. Nugaz aka Antonio Nugaz wa tatu kutoka kushoto wengine
ni Geofrey Meena Meneja Masoko wa TTB na Devotha Mdachi Mkurugenzi wa
Masoko wa pili kutoka kushoto.
Bodi
ya Utalii Tanzania TTB leo imetoa vyeti kwa watanzania watatu
walioipeperusha vyema bendera ya Tanzania katika masuala ya Utalii.
Mkurugenzi
wa Bodi ya Utalii nchini Tanzania Dk Aloyce Nzuki Akizungumza na
waandishi wa habari kwa ajili ya tukio muhimu la kuwatunikia vyeti
watanzania wa tatu amesema watanzania hao waliweza kupeperusha bendera
ya Tanzania vizuri hasa katika masuala ya utalii, kwa hapa Tanzania na
nchi za nje.
Watanzania
hawa wameweza kufanya mambo makubwa ambayo kwa kiasi kikubwa sana
yamechangia kwenye sekta ya utalii.Watanzania ambao tunaowapa tuzo leo
ni pamoja na
- Mr. Respicias H. Baitwa
- Mr. Wilfred Moshi
- Mr. Juma K. Nugaz
1.
Mr. Respicius BaitwaNi mtanzania wa kwanza ambaye ameweka rekodi ya
Afrika kwa mwafrika wa kwanza anatarajia kupanda vilele saba virefu
katika mabara yalioko duniani. Mr. Baitwa mpaka sasa ameshapanda vilele
4. Ameshapanda kilele cha kwanza Mt. Kilimanjaro zaidi ya mara 100,
amepanda Elbrus kilele kirefu katika nchi za ulaya, Aconcagua, Argentina
na Kosciusko Australia.
- 2. Mr. Wilfred Moshi
Wilfred
Moshi amekuwa mtanzania wa kwanza kupanda kilele kirefu kuliko vyote
duniani kilele cha mlima Everest. Wilifred Mosha alipanda mlima Everest
mwezi may 2012 na amekua mwafrika wa 3 kupanda na kufika kilele cha
mlima Everest, na kupandisha bendera ya Tanzania kwa kufanya hivyo
Wilifred Mosha ameweza kutangaza jina la Tanzania na kwenye mahojiano
mbalimbali na vyombo vya habari duniani ameweza kutangaza vivutio vya
utalii wa Tanzania kwa ujumla wake.
3. Mr. Juma K. Nugaz (Antonio Nugaz)
Juma
Nugaz mtayarishaji wa kipindi cha utalii cha Kambi Popote
kinachorushwa na clouds TV amekuwa mtangazaji bora katika kuhakikisha
utalii wa ndani kwa mwaka 2012 tuzo iliytolewa na chama cha waandishi
wa habari Tanzania.
Mr.
Juma Nugaz amekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha utalii wa ndani
kupitia kipindi cha kambi popote na amekuwa akitembelea bila kuchoka
vivutio vya utalii na mwaka jana mwezi wa Disemba aliweza kurekodi
kipindi maalum wakati wa zoezi la kupanda mlima kwa baadhi ya watanzania
katika sherehe za kuazimisha miaka hamsimi (50) wa Tanzania bara ya
Uhuru.Tunampongeza sana.
Bodi ya utalii Tanzania inawapongeza watanzania hawa kwa kufanya
juhudi kubwa ya kutangaza vivutio vyetu vya utalii wa Tanzania na
tutaendea kushirikiana nao kutangaza vivutio vyetu zaidi.
Pamoja
na kuwazawadia cheti hiki vilevile tunawazawadia safari ya kitalii
kwenda mbuga za wanyama za Selous kwa siku nne na familia zao.
Chanzo: http://tabianchi.blogspot.com
No comments:
Post a Comment