Gary baada ya kumpiga Amante risasi akijua amemuuwa, alienda kwa Alvira
huku akijifanya amelewa. Gary anatamka neno moja ambalo linamshtua
Alvira alisema “hakuna kitu kingine kitakacho tuingilia katika maisha
yetu”, lakini bado wakiwa wanaongea, bibi wa Amante alimpigia simu
akimwambia Amante amepigwa risasi, wanaagana na Gary huku nyuma Alvira
akimwaga machozi.
Suzan na MARA na Derick wanafanikiwa kurejea jijini, lakini wanapokea
Ujumbe mbaya wa Amante kupigwa risasi. MARA na Suzan wanafika
nyumbani. Mama yake Gary anawaonyesha kitu kwa kusonta huku akiwa
amejawa na uchu wa kusema kitu, lakini wakati aking’ang’ana kuwaonyesha,
Clara anaingia na kuanza kujibizana na vibaya na MARA. MARA namwambia
Clara “sikujua kuwa wewe na baba yako Gary mnahusika na kutaka kumuuwa
baba yangu, sasa basi wewe na huyo baba yako mtakwenda wote jere”.
Vilio vya tanda hospitali baada ya Alvira kufika hospitali kumuona mumewe Amante, kiukweli anajuta na kutubu kwa makosa yote aliyomtendea mumewe. Lakini wakati akizungumza maneno hayo, tayari Gary alikuwa kajibanza sehemu akitazama picha yote, kitu kinachomfanya aghadhabike maradufu na kuanza kupiga ngumi ukuta. Jamaa anaamua kurejea nyumbani akiwa ni mwenye hasira, anamkuta Clara na kumweleza kuhusu Alvira, lakini kibaya zaidi Clara anamwambia kuwa “nilikwambia mapema kuwa mama hakupendi” maneno hayo yalimuongezea Gary hasira na kujikuta akimkaba shingo Clara.
Alvira anampigia simu Suzan na kudai kuongea na MARA, alishindwa
kuongea bali alimwambia kuwa hali ya baba yake ni mbaya huku akimwaga
machozi kama mvua. Gary pia nampigia simu Alvira na kumueleza kuwa yuko
nyumbani anakula good time, japokuwa alimtaka arejee nyumbani.
Gary anamkuta Clara akiwa anaelekezwa nje na bibi yake kwa
kumnyooshea kidole nje. Gary anang’amua eneo zilipofichwa pesa na
kuzifukua pesa hizo zilizokuwa zimechimbiwa na bibi huyo. Tayari Clara
amekwisha fanya shoping na kurejea nyumbani, lakini bibi yake anamuomba
Clara awasaidie MARA na Suzan, lakini Clara anakataa.
Alvira anarejea nyumbani na kumkuta Gary, Alvira anaulizwa kuwa
alikuwa wapi? Lakini Gary anajibu mwenyewe “unatoka kwa Amante!” Alvira
kwa jazba anamjibu kuwa “ninae mpenda ni Amante sio wewe”, anakimbia
kujifungia ndani huku akiomba msaada kwani Gary tayari alikuwa
kashikilia bastora. Gary anabomoa mlango na kumkamata mkono kwanguvu
Alvira. Alvira kwa hasira anazidi kumuambia hampendi na anamchukia kwani
anampenda Amante.
Alvira akiwa anapiga kelele za kuomba msaada, MARA na Suzan walikuwa
wamefika nyumbani kwa Alvira na kusikia kelele, wote wanawafuata huko
chumbani. Gary kuona hivyo, anatoa bastora na kumnyoshea Suzan lakini
Alvira na MARA wanamzingira Suzan kwa pamoja, lakini Gary bado akiwa na
hasira anawauliza “mnafikiri mtakimbia kwenda wapi?” anawanyooshea
bastora wote watatu. Wakiwa bado wanajibizana maaskali wanafika, na
Avira anawaamuru wamkamate, anakamatwa na kuwekwa ndani.
Huko hospitalini Amante anapata nafuu na kumuulizia Alvira. Clara
afanikiwa kufika hospitali kumuona Amante,Je Clara analipi la kufanya
ilihali baba yake Gary yuko rumande? Je Gary ataendelea kukaa rumande?
Mwandishi: Vikta Machota (Asili Yetu Tanzania)
To be continue..
No comments:
Post a Comment